Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametua
bungeni mjini Dodoma leo kuongoza kikao ambacho pamoja na mambo mengine
kitatoa msimamo wa wabunge wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa),
kushiriki au kutoshiriki vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea na
vikao vyake mjini humo.
Mbowe
pamoja Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ambao pia ni
miongoni mwa viongozi wa chama hicho waliopata dhamana jana katika kesi
ya uchochezi inayowakabili viongozi saba wa chama hicho, wamewasili
bungeni leo mchama na kuingia moja kwa moja katika Ukumbi wa Msekwa kwa
ajili ya kikao hicho.
Baadhi
ya wabunge wamesema kikao hicho kinatarajia kutoa hatma ya kambi hiyo
kushiriki mkutano huu wa Bunge la Bajeti na masuala mengine ambayo
yatatikisa.
Post a Comment
karibu kwa maoni