Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan amewaagiza Waganga Wakuu na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau
mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima
saratani ya matiti na ya mlango wa kizazi.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga
Saratani ya Mlango wa Kizazi mkoani Dar es Salaam ambapo hafla ya
uzinduzi zilifanyika kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala, wilaya ya
Temeke.
Makamu
wa Rais amesema Utoaji wa Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi
pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja vitasaidia kuwakinga mabinti na
kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake na hivyo kuepusha
maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzailika
“
Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe tumewafikia wanawake milioni tatu.
Hii itawezekana endapo kila mmoja wetu ataweka kipaumbele katika kufikia
lengo hilo.” Alisisitiza Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais amesema kuwa Serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya
mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za
chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi.
Makamu
wa Rais aliendelea kusema kuwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ni
walengwa wa kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa
mwaka huu 2018 ambapo jumla ya wasichana 6,16,734.
Makamu
wa Rais ambaye aliwaeleza wananchi waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya
uzinduzi kuwa anaunga mkono uwepo wa chanjo hiyo huku akitoa sababu
mbili moja ikiwa ni kulinda jeshi la wanawake nchini Tanzania kwani
wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao kwa sababu ya Saratani na sababu ya
pili ni kwamba Mama yake Mzazi alifariki kwa kansa hiyo ya saratani ya
mlango wa kizazi.
Wakati
huo huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania imeandika historia nyingine
katika sekta ya afya kwa kuzindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango
wa Kizazi.
Post a Comment
karibu kwa maoni