Aidha, amesema hakuna idadi kubwa ya kutosha kwa askari polisi wa kulinda mikutano ya vyama vya siasa.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni, alisema hayo
jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkoani (CUF),
Twahir Awesu Mohamed.
Katika swali lake, mbunge huyo alihoji ni kwa nini polisi waliwalinda wanachama wa CCM waliofanya maandamano makubwa hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Katika swali lake, mbunge huyo alihoji ni kwa nini polisi waliwalinda wanachama wa CCM waliofanya maandamano makubwa hivi karibuni visiwani Zanzibar.
“Kumekuwa
na katazo la kufanya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa lakini
Aprili 8, mwaka huu, CCM mikoa miwili ya Pemba waliandamana chini ya
ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi wakiwa wamebeba mabango wakiimba nyimbo
za kuhalalisha amani na uchochezi. Hili katazo linahusu vyama vya
upinzani pekee au vyama vyote?” alihoji.
Aidha
katika swali la msingi, mbunge huyo alihoji ni lini jeshi la polisi
litafanya kazi zake kisayansi zaidi na kuondokana na kutumia nguvu
zisizo za lazima wakati wa kutekeleza majukumu yake
“Suala
la weledi kwa watendaji wa polisi linasimamiwa vipi ili polisi waweze
kupambana na uhalifu unaokuwa kitaalam kila siku,”alihoji.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri Masauni alisema suala la kuandamana kama yameruhusiwa lazima jeshi la polisi litoe ulinzi.
“Kipindi
hicho ambacho serikali ina shughuli nyingi za kiuchumi, jeshi la polisi
haliwezi kuendekeza kutoa ulinzi katika maandamano au mikutano kwa kuwa
hatuna askari wa kutosha wa kufanya shughuli hizo,”alisema.
Alisema kwa taasisi au chombo chochote kitakachohitaji kufanya maandamano au mikutano jeshi la polisi halina muda huo.
Alisisitiza kuwa sheria ni msumeno inakata kote kote hivyo ni vyema sheria zikafuatwa.
Alifafanua kuwa katika kutekeleza kazi zake polisi anaruhusiwa kutumia nguvu inayoendana na mazingira ya tukio
Aidha
alisema serikali imekuwa ikiwajengea uwezo wa kiutendaji askari kwa
kutoa mafunzo mbalimbali sehemu za kazi yenye lengo la kuwakumbusha
taratibu za kazi.
Alifafanua
kuwa katika kuhakikisha linafanya kazi kwa weledi jeshi la polisi
limekuwa likiajiri wasomi wenye taaluma mbalimbali kama vile teknolojia
ya habari na mawasiliano (Tehama), maabara, uchunguzi wa nyaraka na
taaluma zingine zinazohusisna na makosa yanayosababishwa na ukuaji wa
teknolojia.
Post a Comment
karibu kwa maoni