Jukwaa
la Wahariri Tanzania (TEF), limetoa wito kwa serikali kufanya
mazungumzo ya kitaifa kwa kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii
kujadili mustakabali wa amani na maridhiano ya kitaifa kabla hayajatokea
makubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Aprili 5,
Kaimu Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deodatus Balile alisema makundi hayo ni
pamoja na wanahabari, viongozi wastaafu, wakuu wa vyama vya siasa na
asasi za kiraia.
Ametaja
makundi mengine ni vyama vya kitaaluma na vya makundi ya rika na
makundi mengine muhimu kukutanishwa pamoja kama Rais John Magufuli
alivyokutana na wafanyabiashara hivi karibuni.
“Hali
ya nchi kwa sasa imekuwa na sintofahamu na malalamiko kutoka katika
makundi mbalimbali jambo ambalo halitaleta afya kwa taifa, mambo mengi
yamekuwa yakilalamikiwa ikiwa ni pamoja na kuminywa kwa uhuru wa kutoa
maoni hasa kupitia vyombo vya habari kuzorota kwa demokrasia, ukuaji wa
uchumi usioakisi hali halisi ya maisha ya watu.
“Tumeamua
kutoa tamko hili leo, baada ya kukutana kwa wahariri jana kujadili
mustakabali wa nchi na mambo yanayoendelea kwa sasa.
“Kuminywa
kwa uhuru wa kutoa maoni imekuwa kikwazo kikubwa cha utendaji na
ufanisi katika vyombo vya habari na kutokuwa huru kwa kutoa taarifa
mbalimbali kama mwanzo na hofu huku ikiwafanya wananchi kusita
kuzungumza,” alisema Balile.
Alisema
mazingira ya kazi kwa wanahabari yamekuwa magumu kutokana na baadhi ya
watendaji wa vyombo vya dola kuwabughudhi na kufanya uovu wa wazi dhidi
yao wanapokuwa kazini.
“Matukio
mbalimbali ya Polisi kuwanyanyasa waandishi Wa habari yakiwamo ya
wanahabari kunyang’anywa simu zao mfano yaliyotokea Dodoma kwa mwandishi
kuporwa simu, kupotea kwa Azory Gwanda wa Mwananchi na kwingineko,”
alisema Balile.
Amesema hali hiyo inawafanya waandishi na wananchi kuwa na hofu hasa kwa wale wa habari za uchunguzi.
“Vyombo
vya habari vimekuwa vikifanya kazi katika mazingira magumu na ya woga
kutokana na watendaji wake kuitwa na kuhojiwa na mamlaka kama vile Idara
ya Habari (Maelezo) na Mawasiliano Tanzania (TCRA).
“Aidha,
vituo vitano vya televisheni kutozwa faini ama kufungiwa vituo vitano
vya televisheni kutozwa faini na TCRA na kufungiwa kwa magazeti, baadhi
ya adhabu zimekuwa zikitolewa kinyume na sheria ya huduma za habari ya
mwaka 2016,” alisema Balile.
Post a Comment
karibu kwa maoni