Wakaazi wa kijiji cha Kiongozi kata ya Maisaka mjini Babati mkoani Manyara wamekataa
maadhimio ya Halmashauri ya Kijiji katika kikao kilichofanyika tarehe 12 mwezi
wa nne mwaka 2018 chini ya mwenyekiti wa Kijiji hicho Thomas Lohay
kuuza mlima kwa mkandarasi Rock Tronick.
Wamesema kuwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha za miradi mbalimbali ya
kijiji,wanahofia hata fedha zitazotokana na mlima huo hazitowasaidia hivyo
hawaoni haja ya kuuzwa na kumueleza mkurugenzi kuwa watafute maeneo mengine ili
nao wanufaike.
Wakieleza malalamiko hayo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Fortunatus
Fwema katika mkutano mkuu wa Kijiji
wameaanisha miradi mbali mbali ambayo haiendani na kiwango cha fedha
zilizotumika wakitolea mfano choo cha shule ya msingi Kiongozi kichogharimu
shilingi million 9,978,000.
Baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi hao, mkurugenzi aliunga mkono
hoja hizo kwa ueleza kuwa mlima huo haotouzwa.
Akizungumzia kuhusu suala la choo kujengwa chini ya kiwango amesema
atawaagiza wataalamu ili kuweza kubaini kama kiasi kilichotumika kinaendana na
ubora wa choo hicho.
Post a Comment
karibu kwa maoni