Rais
mpya wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Fatma Karume
aliyechaguliwa kwa kishindo wikendi hii, amesema katika kipindi chake
atahakikisha anashughulikia zaidi suala la utawala wa sheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, muda mfupi baada ya kuchaguliwa kushika
nafasi hiyo akipokea kijiti kutoka kwa Tundu Lissu, Fatma amesema kuwa
moja kati ya suala linalolalamikiwa na wanachama wengi ni watu
kushikiliwa mahabusu kwa muda mrefu bila kupelekwa mahakamani.
“Wanachama
wetu wametaka tushughulikie suala la watu kushikiliwa kwa miaka mingi
bila kupelekwa mahakamani. DPP anasema bado upelelezi haujakamilika.
Sasa wanataka watu wasiendelee kushikiliwa kama upelelezi bado
haujakamilika au wafikishwe mahakamani,” alisema.
Akizungumzia
tathmini yake kwa mtangulizi wake, alisema alifanya kazi nzuri katika
kipindi kifupi alichokuwa ofisini lakini pia hata baada ya kupata
matatizo makamu wake aliendelea kufanya kazi nzuri pia.
Fatma
ameahidi kutumia nafasi hiyo kuhuisha utawala wa sheria nchini na
kuepuka baadhi ya viongozi kufanya kazi kwa kufuata matamko kinyume cha
matakwa ya katiba.
Mwanasiasa
huyo alipigiwa kura 820 akimuacha kwa mbali Ngwilimi aliyemfuatia
akipata kura 363, Mwapongo kura 12 na Wasonga akipata kura 6 kati ya
kura 1,195 zilizopigwa na kuhesabiwa. Kipindi chake cha urais
kitakamilika baada ya mwaka mmoja.
Post a Comment
karibu kwa maoni