Jeshi la polisi Mkoa wa Manyara limewatahadharisha wenye nia
ya kutaka kufanya maandamano yanayohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii na
watu wachache wenye nia mbaya na taifa.
Akizungumza leo wakati
wa mazoezi ya utayari Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga
amesema kuwa jeshi hilo lipo tayari kwa kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa
amani na kwamba yeyote atakaethubutu hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu
yake.
Kwa mujibu wa taarifa za mitandaoni ni Kwamba Mange Kimambi, mwanamitindo
aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa siasa, ndie muasisi wa maandamano yanayaopangwa
nchi nzima kupinga kile anachokiita kuwa ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki za
binadamu na uminywaji wa haki za kiraia nchini Tanzania.
Maaandamano hayo yamepangwa kufanyika katika siku ya
kumbukumbu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sherehe ambazo zinatarajiwa
kufanyika mkoani Dodoma Kitaifa na kuhutubiwa na Rais John Pombe Magufuli.
Afisa mtendaji wa kata ya Mutuka akitoa maoni yake kuhusu
vugu vugu hilo la maandamano amesema kuwa endapo watu watafanya hivyo watatoa
mwanya kwa wahalifu kuvunja sheria kiurahisi.
Post a Comment
karibu kwa maoni