0
Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul amesema wakuu wa mikoa ambao wametolewa kwenye vyama vya siasa wanafanya mambo ya ajabu katika maeneo yao ya kazi.

“Mimi nataka nibomoke, sitaki kuumia kifua....Hawa wakuu wa mikoa wanaoteuliwa bila kuangalia wamehudumia katika utumishi wa umma kwa muda gani, wanafanya mambo ya ajabu,”amesema.

Gekul ameyasema hayo Jana Aprili 12, bungeni na kumuomba Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ‘abomoke’ bungeni akimaanisha kuongea yaliyo moyoni mwake wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Gekul amesema kuwa viongozi wa wilaya na halmashauri kuanzia Hanang, Tunduma na kwingineko wanafanya kazi ya kisiasa na si maendeleo.

“Ni maeneo yote kuanzia Hanang ambako hata mzoefu Mama Nagu anawekwa ndani, wanafanya kazi ya siasa na sio kazi ya maendeleo,” amesema.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top