Mke wa nane wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III), Senteni Masango amefariki dunia akiwa chumbani kwake wikiendi iliyopita.
Vyombo
vya habari nchini Swaziland vimeeleza kuwa Bi. Masango alitumia dawa
aina ya AMITRIPTYLINE kupita kiasi (Overdose) kitu ambacho kimepelekea
mwanamke huyo kupoteza masiha, hii ni baada ya mwili wake kufanyiwa
uchunguzi na madaktari nchini humo.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Face 2 Face umeeleza kuwa Bi. Masango alichukua
uamuzi huo wa kujiua Ijumaa ya Aprili 07 ya wiki iliyopita, Baada ya
mumewe kumkataza kuhudhuria kwenye mazishi ya dada yake yaliyofanyika
Jumapili ya Aprili 01, 2018.
Kufuatia
tukio hilo, tayari serikali nchini Swaziland kupitia kwa Waziri Mkuu wa
nchi hiyo, Dkt. Sibusiso Dlamini imetuma salamu za rambi rambi kwa
familia ya Mfalme Mswati (III).
Bi.
Masango aliolewa na Mswati (III) mwaka 1999 na ameacha watoto wawili wa
kike na leo Aprili 10, 2018 mwili wake unatarajiwa kuzikwa kwa heshima
nchini humo.
Post a Comment
karibu kwa maoni