Mahakama
ya Wilaya ya Dodoma, imemfutia mashtaka ya kutaka kujiua na kuamuru
akapatiwe matibabu ya afya ya akili katika Taasisi ya Mirembe Isanga,
mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma, Onesmo Machibya (44),
maarufu kama ‘Nabii Tito’.
Mahakama
hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti za vipimo vya afya ya
akili ya Nabii Tito kutoka Mirembe Isanga, vinavyothibitisha kuwa ana
ugonjwa wa akili.
Awali,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Kalayemaha, aliagiza kuwa
Nabii Tito apelekwe katika taasisi hiyo ya magonjwa ya akili ili
kupatiwa matibabu ya afya ya akili na mahakama imemwondelea mashitaka
yaliyokuwa yakimkabili.
Alisema
katika ripoti ya kitabibu inaonyesha kuwa Nabii Tito kweli ana matatizo
ya afya ya akili, hivyo anatakiwa kupelekwa katika taasisi hiyo ya
Isanga Mirembe ili kupatiwa matibabu.
Mahakama
hiyo, Februari 5, mwaka huu, iliamuru kuwasilishwa kwa vielelezo
vinavyoonesha Nabii Tito ana matatizo ya akili na kufanyiwa vipimo
katika Taasisi ya Afya ya Akili Mirembe Isanga kutokana na mshitakiwa
kudai kuwa ana matatizo ya akili.
Akitoa
maelezo ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
James Karayemaha, Wakili wa Serikali, Beatrice Nsana, aliiomba mahakama
kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuwasilishwa kwa taarifa
kutoka Isanga.
Kutokana na maombi hayo, Hakimu Karayemaha alimuuliza mshtakiwa kama amekuja na vielelezo kama alivyoamriwa na mahakama hiyo.
Mshtakiwa
huyo alimwambia Hakimu kuwa ametekeleza amri hiyo na kwamba tangu amri
hiyo itolewe amekuwa mahabusu na hajapelekwa kwenye taasisi hiyo ya
Isanga.
Hata
hivyo, Hakimu Karayemaha alisema mshtakiwa huyo amewasilisha vielelezo
vyake kutoka Hospitali ya Taifa ya Mhimbili na kwamba mahakama inahitaji
taarifa kutoka Taasisi ya Mirembe Isanga kama ilivyoagiza.
“Mahakama
ilitoa amri apelekwe Taasisi ya Mirembe Isanga kwa mujibu wa kifungu
namba 219 (2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,” alisema Hakimu
hiyo.
Kifungu
hicho kinasema kama mshtakiwa atabainika kuwa kweli ana matatizo ya
afya ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na
akili timamu hivyo hana hatia.
Kutokana
na hali hiyo, Hakimu Karayemaha alimwamuru Mkuu wa Magereza ya Isanga
kutekeleza amri ya Mahakama iliyotolewa ya kumpeleka kufanyiwa vipimo
mshitakiwa huyo.
“Namwamuru
Mkuu wa Magereza Isanga atekeleze amri ya mahakama ili taarifa za
mshtakiwa ziletwe kwa tarehe itakayopangwa ambayo ni Machi 5, mwaka huu,
tutataja kesi na kupokea taarifa ya vielelezo vya vipimo vyake kutoka
Isanga,” alisema Hakimu.
Nabii
Tito alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na
wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu katika
mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.
Post a Comment
karibu kwa maoni