Rais John
Pombe Magufuli ameiagiza wizara ya maji,vyombo
vya ulinzi na usalama kuchunguza na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote
waliohusika na upotevu wa shilingi Bilioni mbili za mradi wa maji wa Ntomboko wilayani Kondoa.
Rais Magufulili
amesema kuwa wahusika wa ubadhirifu huo watafutwe popote walipo wakamilishe
mradio huo au warudishe fedha hizo.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo April 24.2018 Bicha Kondoa alipokuwa akizungumza na wananchi
wa Dodoma na Manyara katika halfa ya uzinduzi wa Bara bara ya Dodoma Babati
yenye urefu wa Kilomita 251.
Rais
Magufuli amesema kuwa wapo watu wasiopenda kuona maendeleo haya yanayofanyika
kwa sababu wamezoea kuwaibia wananchi lakini kwa sasa serikali yake haitokubali
hali hiyo na kuwataka wananchi wa Manyara na Dodoma kutembea kifua mbele kwa
kujivunia Maendeleo.
Walipopata nafasi ya kuzungumza wabunge wa mjimbo manne waliokuwepo kwenye hafla ya uzinduzi wa bara bara,Miongoni mwa wabunge walisimama na kuzungumza ni wa jimbo la Babati mjini [CHADEMA] Pauline Gekul ambapo mbali na kutoa pongezi kwa mradi huo wa bara bara kwa kiwango cha Lami alimuomba Rais Magufuli kuirudisha stendi ya Babati kwa Halmashauri kutoka CCM kwani ndio tegemeo la
Halmashauri.
Akijibu hilo
Rais Magufuli amesema viongozi wa Babati wakae chini na kutatua migogoro
iliyopo kwa kuwa nchi ni kubwa sio kila tatizo yeye atatue.
Post a Comment
karibu kwa maoni