0
Image result for UPUPU 
Waalimu watatu wa Shuleya Msingi Kimamba B iliyopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wanadaiwa ku mpigamwanafunzi wadarasa la 4 mwenye umri wa miaka 10 na kumsababishia kulazwa
katika taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) Jijini Dar esSalaam.
Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo,Bi. Phily Muhebi mkazi wa Kilosa amesema kuwa mwanaye alijeruhiwa vibaya kwa
kipigo kutoka kwa waalimu hao  Machi 19, mwaka huu kwa kosa aliloelezwa na wanafunzi wenzake kuwa ni baada ya mwenzake mmoja kulalamika kwa walimu kuwaamempaka upupu.
Taarifa za kujeruhiwa kwa mtoto huyozimefikishwa Polisi huku Mama huyu akilalamikia vitisho alivyopewa na MwalimuMkuu wa Shule hiyo licha ya mwanaye kuumizwa vibaya na walimu wake.
Mama wa Mtoto huyo amesema kwa sasaanahangaikia matibabu ya mwanaye huyo huku akihofia uwezo wake wa kumudugharama za matibabu, ambapo ameiomba Wizara ya Elimu kuingilia kati suala hilo sambamba na kuwezesha upatikanaji wa haki dhidi ya unyama aliofanyiwa mwanaye.
Uchunguzi wa Afya mtoto huyounaendelea, huku taasisi ya mifupa MOI ikiiahidi kutoa tarifa kamili punde baada ya uchunguzi wa kina wa kitabibu wanaoufanya utakapokamilika.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top