
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe
01 Aprili, 2018 ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho
ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Misa hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Padre Venance Tegete.
Akizungumza
baada ya kukaribishwa na Padre Tegete kutoa salamu, Mhe. Rais Magufuli
amewatakia Watanzania wote heri ya Pasaka na ametoa wito kwa Watanzania
kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika
ujenzi wa Taifa.
“Kifo
na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo ukafufue matendo yetu, tuendelee
kuijenga amani yetu, upendo wetu na tujenge maendeleo ya Watanzania
wote, kwani Kristo alifundisha upendo miongoni mwetu.
“Kwa
hiyo Baba nakushukuru sana kwa kuongoza Misa hii, naomba ufikishe
shukrani zangu kwa Kardinali Pengo, Maaskofu wote na Watanzania wote
tuendelee kusimama pamoja ili kulijenga Taifa letu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli aliongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam
01 Aprili, 2018


Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.