
Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Mdee
amekamatwa leo alfajiri uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
akitokea nchini Afrika Kusini inakoelezwa alilazwa kwa matibabu.
Meya
wa Ubungo, Boniface Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Halima Mdee
ambapo amesema; "Ni kweli amekamatwa leo Saa 9 alfajiri Airport,
akitokea Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu na sasa yupo
Central."
Mdee
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha)
huenda akaunganishwa na vigogo wengine sita akiwamo Mwenyekiti wa Chama
hicho, Freeman Mbowe katika kesi inayowakabili.
Vigogo
hao wengine tayari wamekwisha kupandishwa kizimbani katika mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka nane.
Kukamatwa
kwa Mdee kunafikisha watuhumiwa saba kati ya nane ambao wamekwisha
kuhojiwa mwingine ambaye bado na huenda anatafutwa na jeshi hilo ni
mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.