Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imesema
katika mikakati yake ya kuwatambua wagonjwa wanaoishi na virusi vya
UKIMWI pamoja na TB wameazimia kutembea maeneo yenye mikusanyiko ya watu
wengi ikiwemo baa, migodini na mahali penngine ili waweze kuwatambua
kiurahisi.
Hayo yameelezwa na serikali ya awamu ya tano kupitia Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Aprili 23, 2018 Bungeni jijini
Dodoma kwenye kikao cha 15 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza kutoka kwa Mbunge
Masoud Abdallah aliyetaka kufahamu serikali ina mikakati gani katika
kutoa elimu maalum ambayo itaweza kuenea kwa kasi zaidi katika maeneo
yenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi.
"Serikali
baada ya kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa
makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na
UKIMWI. Hivyo tumeamua kujielekeza kutoa elimu kwa njia mbalimbali
ikiwemo vyombo vya habari lakini vilevile tuna mkakati mahususi wa
kuwatafuta wagonjwa wa TB katika migodi sambamba na hilo tumetengeneza
tumetengeneza mikakati jumuishi kati ya ugonjwa wa TB na UKIMWI", amesema Dkt. Ndugulile.
Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "sasa
hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata
kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar.
Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa
suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB".
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile
amesema kumgundua mgonjwa wa TB mapema na kumuweka katika matibabu ndio
njia kuu ya kupambana na kulishinda tatizo la kifua kikuu jambo ambalo
lipo kwenye mikakati ya serikali katika kufufua uwezo wa kufikia watu
wote wanaohitaji huduma za TB ili kuwagundua mapema na kuwatibu
kikamilifu.
Post a Comment
karibu kwa maoni