Tanzania
inatarajia kuungana na nchi zingine duniani kwenye kuadhimisha siku ya
Malaria Duniani ambayo ufanyika April 25 kila mwaka.
Maadhimisho
hayo ya kitaifa yatafanyika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma huku Waziri
wa Afya na Maendeleo ya Jamii akitarajiwa kuzindua ripoti ya hali ya
Malaria nchini.
Akiongea
jijini Dar es Salaam, Waziri Nyoni ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi
kutoka VectorWorks alisema kutakuwa na shamra shamra mbali mbali kuanzia
tarehe 22 April kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo.
VectorWorks
ni mradi wa miaka mitano wa kupamba na malaria hapa nchini umefadhiliwa
na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kupitia Mfuko wa Raisi wa
Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na John Hopkins Center for
Communications.
“Sisi
kazi yetu ni kuhakikisha hali ya ugonjwa wa malaria inapungua. Kwa
sababu hiyo, tumekuwa na zoezi endelevu la kugawa vyandarua vyenye dawa
ya muda mrefu kwa kila kaya hapa nchini. Vile vile, tunatumia vituo vya
afya kuwafikia walengwa wakuu ambao ni akinamama waoenda kliniki na
watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja,” alisema Nyoni.
Akina
mama wanaonza kliniki ni lazima wapatiwe chandarua chenye dawa ya muda
mrefu bure. Hii njia bora ya kujikinga na mbu waenezao malaria. Vile
vile tunafanya kazi kwa kushirikiani na Serikali kupitia Wizara ya Afya
kitengo cha kupamba na Malaria nchini ambao wamekuwa wakipuliza dawa
yenye viatilifu kwenye maeneo yenye masalia ya mbu.
“Tumepiga
hatua kubwa kupunguza malaria hapa Tanzania kwa hivyo natoa wito wangu
kwa kila Mtanzania kuhakikisha analala kwenye chandarua kwenye dawa ya
muda mrefu,” aliongeza Nyoni.
Post a Comment
karibu kwa maoni