
Shirika la Anga la Ulaya, ESA, limesogeza nyuma muda ambao chombo cha
anga za juu cha China kinatarajiwa kuingia katika anga la dunia, ambao
ni kati ya Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi. Chombo hicho, Tiangong-1,
kilipelekwa angani mwaka 2011, na hakiwezi kurejeshwa duniani chini ya
uangalizi wa wanasayansi kwa sababu kiliharibika miaka miwili iliyopita.
Awali chombo hicho kilitarajiwa kuingia duniani Jumapili jioni, lakini
hali ya anga ilibadilika ghafla na kupunguza kasi yake. Wanasayansi
wanatabiri kuwa Tiangong itaungua moto punde tu ikiingia katika anga la
dunia, lakini baadhi ya vipande vyake vitaanguka duniani, vikitapakaa
katika eneo la kilomita nyingi za mraba. Wataalamu hao wanabashiri kuwa
kuna uwezekano mkubwa kwamba vipande vivyo vitaanguka baharini. Chombo
hicho kina uzito wa tani 8.5.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.