Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amewataka askari wa
Kikosi cha Usalama Barabarani kujitafakari kuhusu faini wanazotoza na
kuacha kubambikiza kesi kwa madereva.
Akijibu
hoja za wabunge walizozitoa wakati wakichangia bajeti ya wizara hiyo
mwaka 2018/19 jana Mei 4, 2018 bungeni mjini Dodoma, Masauni amesema
chanzo kikubwa cha ajali barabarani ni pamoja na makosa ya kibinadamu
kwa asilimia 76, ubovu wa miundombinu na uchakavu wa magari.
“Bado
kuna changamoto za baadhi ya madereva ambao hawafuati sheria. Trafiki
acheni tabia za aina hiyo, watu hawajafunga mkanda badala ya
kumwelewesha unamtoza faini,”alisema.
“Lazima
waangalie uzito wa kosa lenyewe na wafanye kwa mujibu wa sheria. Kama
mtu hajafunga mkanda unamtoza faini badala ya kumpa elimu tu. Raia nao
wawape ushirikiano askari wetu kwani wanafanaya kazi katika mazingira
magumu zaidi.”
Amlisema
serikali kwa upande wake inafanya kila juhudi ikiwemo kupata mkopo
mkubwa kutoka Benki ya Exim wa Sh500 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba za Serikali ambapo kila nyumba itajengwa kwa gharama ya Sh25
milioni.
Kuhusu
uhamiaji, Masauni amesema Serikali imefanikiwa kufumua mtandao wa
watendaji wa idara ya uhamiaji mikoani ambao hawakuwa waaminifu katika
utendaji wao wa kazi.
Ameahidi
kufanya kila namna ya kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao
wamekuwa wakilalamika kuhusu utendaji wa idara hiyo kwa kila wakati
kuulizwa kuhusu vitambulisho.
Post a Comment
karibu kwa maoni