Waliofariki
katika ajali hiyo ya kusikitisha ni Chrispin Senga mwenye umri wa miaka
40, Salome Chaulinge mwenye umri wa miaka 31 na Mtoto wao Paulina Senga
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo limetokea
jana, Mei 29 saa 6 mchana katika eneo la kituo cha mafuta cha Munio,
mjini hapa.
Kamanda
Kyando amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Saratoga
lenye namba T 211 AED aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Ally
Fabiano (31) mkazi wa Kigoma.
“Basi
hilo lilikuwa likitokea Sumbawanga mjini kuelekea mkoani Kigoma na
wanafamilia hao walikuwa wamepanda pikipiki yao aliyokuwa akiendesha
Senga,” amesema Kyando.
Kamanda
wa polisi amesema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea ilikuwa vigumu
kuitambua miili ya wazazi kwani iliharibika vibaya ila kichwa cha mtoto
peke yake ndio kilionekana.
“Ilikuwa
vigumu hata kuitambua miili ya wale wazazi wa mtoto paulina kwani
aliharibika vibaya lakini mtoto peke yake ndio kichwa kilionekana.”
amesema Kyando.
Post a Comment
karibu kwa maoni