Hali ya
Ukeketaji katika mkoa wa Manyara bado ni tatizo kutokana na watoto wchanga pia
kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa siri pale wanapozaliwa.
Anna
Emmanuel Fisoo afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Manyara anaeleza kuwa tatizo la
ukeketaji kwa wanawake na watoto bado lipo katika maeneo mengi ya mkoa katika
baadhi ya makabila ya wafugaji.
Amesema
ukatili mwingine wanaofanyiwa watoto ni ulawiti na kubakwa na kwamba kesi
nyingi zipo Mahakamani.
Amesema ili
kutokomeza ukatili huo ni lazima jamii,taasisi za serikali na mashirika binafsi
kila mmoja atimize wajibu wake kwa wakati na kwa kufanya hivyo hali hiyo
itakuwa imepungua kwa asiliamia 50 ifikapo mwka 2022.
Paskalia
Changala Mratibu wa shirika linalojishughulisha na masuala ya kutokomeza
ukeketaji kwa watoto wa kike na ukatili wa kijinsia [AFNET]anasema hali ya
Ukeketaji mkoa wa Manyara kwa takwimu ipo juu kwa asilimia 70.8 na kwa sasa
watu wamegundua mbinu mpya ya kufanya
ukeketaji kwa kuwakeketa watoto wachanga.
Aliendelea kusema kwa kusema “zamani walikuwa
wakikeketa wakiwa wakubwa lakini kwa sasa wamebadilisha njia”alisema Changala.
Aidha
Changala anasema wao kama AFNET wamekuwa wakishirikiana na Serikali kupitia
ofisi ya jinsia na Maendeleo ya jamii pamoja na Dawati la jinsia Polisi kutoa
elimu kupitia mikutano ya hadhara na mashuleni pamoja na kuwakusanya Mangariba
ambao kwa sasa ndio wakunga wa jadi.
Shirika hilo
limewataka wanaofanya kazi hiyo waachane
nayo mara moja,watafute mawazo mbadala ya kuwaingizia kipato na sio kutumia
viungo vya binadamu.
Wasichana
wengi wamekuwa wakipoteza maisha baada ya kufanyiwa Ukeketaji kwa sababu ya
kuvuja damu nyingi hivyo basi WALTER HABARI inaiomba jamii zinazofanya vitendo
hivyo ziache na kutii wito wa serikali
wa kuacha kukeketa.
Mangariba
hao wamekuwa wakipatiwa vitu kama vile mbuzi,ng’ombe na Kondoo na vitu
vingine kama ujira baada ya kufanya
kitendo hicho cha ukeketaji kwa wasichana.
Kumbuka
Ukeketaji unamnyima haki na uhuru Msichana.
Post a Comment
karibu kwa maoni