Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempigia
simu Katibu Mkuu wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo mbele ya wananchi wa
kijiji cha kidodi , kumtaka kumchukulia hatua mkandarasi aliyepewa
mradi wa maji na kutoukamilisha.
Akizungumza
kwa sauti kubwa huku wananchi wa Kidodi wakiwa wanasikiliza 'live',
Rais Magufuli amesema kwamba mkandarasi huyo alishapewa pesa za mradi
milioni 800 lakini maji hayajafika kwa wananchi, hivyo ahakikishe
amechukuliwa hatua za kisheria au awepo eneo la mradi kukamilisha.
Awali
kabla ya kupiga simu hiyo, Rais Magufuli ametuma salamu kwa mkandarasi
huyo kupitia wananchi wa kijiji cha Kidodi, kumtaka azirejeshe fedha
alizopewa za mradi pasipo kutekeleza mradi huo muhimu kwa jamii.
“Nafahamu
kuna mradi wa maji wa milioni 800 na mkandarasi alipewa, lakini maji
hayajafika kwa wananchi, nilidhani mbunge wenu atauliza achukuliwe hatua
gani lakini hajauliza, na mkandarasi kama alikula hela atazitapika,
naomba mumfikishie huu ujumbe”, amesema Rais Magufuli.
Baada
ya simu hiyo Profesa Mkumbo amesema anatarajia kuanza safari mchana huu
kwenda kijijini hapo kushughulikia tatizo hilo, na mpaka kesho atakuwa
ameshafika eneo la tukio na kutoa suluhu.
Post a Comment
karibu kwa maoni