0
Image may contain: 1 person, sitting

Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imejiwekea mikakati ya kumaliza tatizo la vyoo katika shule za Msingi na Sekondari ifikapo mwezi July mwaka huu.

Hayo ameyazungumza mkuu wa wilaya ya Babati Mhandisi Raymond Mushi akitoa taarifa ya serikali kwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati  kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Amebainisha kuwa Shule za msingi Babati zina upungufu wa matundu ya vyoo  938 wakati kwa upande wa sekondari ni matundu 227.


Mkuu wa wilaya amesema kuwa mkakati uliopo kwa sasa ni kuhakikisha kila shule kwa kutumia  nguvu zao  inakuwa na matundu ya vyoo ya kutosha na Halmashuri itamalizia pale watakapofikia.

Kwa upande wake mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Malinga amesema kwa sasa kinachofanyika ni kupitia kila shule na kutambua idadi ya matundu ya vyoo yanayohitajika pamoja na kiasi cha fedha kitakachohitajika.

Akizungumzia matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu na wasichana ameeleza kuwa katika halmashauri yake hilo linafanyiwa kazi na lilishaanza tangu mwaka jana.

Hata huvyo ameeleza kuwa mkakati wa serikali pamoja na wananchi ni kutaka kuondoa tatizo hilo kupitia michango ya hiari.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top