Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga amewaomba radhi Watanzania kwa tukio alilolifanya la 'kujigeuza daktari.'
Mlinga amesema aliitwa kuhudhuria uzinduzi wa chanjo na wala yeye si mtaalamu wa afya.
"Kitaalamu
mimi ni mtawala si daktari, nilifanya nilivyoelekezwa na sikufahamu
madhara yake wanasema kitabibu huruhusiwi kushika hata sindano," amesema
Mlinga na kuongeza:
"Kuomba msamaha si woga, sisi tulioendelea nasema kunradhi."
Mlinga
amesema hayo baada ya picha yake kuzagaa katika mitandao ya kijamii
ikimuonesha anamdunga sindano binti wakati wa uzinduzi wa chanjo ya
kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana jimboni mwake.
Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu alizungumzia suala hilo bungeni na kusema ingawa
viongozi hao hawakuwachoma sindano lakini ni makosa kushika hata
sindano.
Post a Comment
karibu kwa maoni