Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga,
Peter Nyalali, amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Utumishi wa halmasahauri
hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa
vijiji 41 licha ya serikali kuagiza warejeshwe.
Nyalali
ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri
hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda
kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.
Hivi
karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote
walioajiriwa kuanzia Mei Mosi, mwaka 2004, ambapo mara baada ya kauli
hiyo Nyalali alimwagiza Dibogo kuwarudisha kazini watendaji hao 41 wa
vijiji.
Pamoja
na kutolewa agizo hilo Kaimu Ofisa huyo Utumishi anadaiwa kutotekeleza
agizo hilo jambo lililomlazimu mkurugenzi kumsimamisha kazi.
Nao
baadhi ya watumishi waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa miezi minane
walitoa shukrani zao kwa serikali na kuahidi kuendelea kuwa wachapakazi.
Mei
2, mwaka 2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea
katika maeneo mbalimbali nchini na baadaye kutoa kibali cha kuajiri
watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka
kujiendeleza wawapo kazini.
Post a Comment
karibu kwa maoni