0
Image result for usalama sc babati
Ligi Ya Mabingwa Wa Mikoa Inaendelea Kupigwa Katika Viwanja Mbali Mbali Hapa Nchini Ambapo Kesho  Wafunga Buti Kutoka Manyara- Babati Usalama Sc Itavaana Na Bingwa Kutoka Mkoani Arusha Bishop Durning Kunatarajiwa Katika Dimba La Ccm Boma Hai Kilimanjaro.
Kwa sasa Usalama Sc imeweka kambi wilayani Simanjiro na kikosi kipo fiti hakina majeruhi kwa mujibu wa Msemaji wa timu Ramadhani Masudi Fupe.
Ikumbukwe Usalama Katika Mechi Ya Ufunguzi Alifanikiwa Kumfunga Uzunguni Ya Boma Hai Mabao 3-1.
Bishop Durning Ambayo Inaenda Kumenyana Na Usalama Sc Jumatano Mei 9.2018 Haina Raha Baada Ya Jana Kulazwa Kwa Bao 1-0 Na Sahare All stars ya Tanga.
Mchezo Huo Ligi Ya Mabingwa Mikoa (RCL) Kundi D yote inapigiwa katika viwanja vya Ccm Boma Hai Kilimanjaro na itakamilika Mei 22 mwaka huu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top