0
May 3 kila mwaka  ni siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari,na kwa mkoa wa Manyara waandishi wa habari wanakutana katika ukumbi wa mikutano ofisi za mkoa huu ambapo Mkuu wa mkoa Alexender Mnyeti anatarajia kuzungumza na wana habari wa vyombo mbalimbali vya habari.
Kauli mbiu ya mwaka huu; UHURU WA WA HABARI IWE NI CHACHU YA UWAJIBIKAJI KWA MAENDELEO YA MKOA'.
Wakizungumza mapema asubuhi katika kipindi cha Tuzungumze na Manyara Fm kinachoendeshwa na John Walter na  Lucas Mondu, Mwenyekiti na Katibu wa klabu ya Waandishi wa Habari Manyara wametoa wito kwa Waandishi wa habari kufanya  kazi kwa kutumia misingi ya Taaluma katika kuielimisha jamii kwa kuwa ni muhimili muhimu unaotegemewa na wengi.
 Katibu wa klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Manyara Tedy Charles [HABARI LEO] anasema 'Waandishi wa habari tunawajibu wa kutumia Taaluma zetu kuandika habari zenye maslahi mapana ya wananchi na zinazozingatia weledi na maadili ya uandishi wa habari na zenye lengo la kuilinda na kuidumisha Tunu ya Amani ya nchi yetu huku wadau wengine tukirahisisha upatikanaji wa habari hizo ili tuwe na mkoa na taifa lenye Maendeleo na linalojitegemea kiuchumi.' Alisema Tedy Charles.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Yusuph Dai [CLOUDS TV] ameeleza kuwa kwa sasa uhuru wa vyombo vya habari na wana habari bado haujasimama akizitaka mamlaka zinazohusika kuhakikisha zinalinda Uhuru wa Habari na wana habari.
Ameendelea kusema kuwa katika mkoa wa Manyara klabu kupitia viongozi waliochaguliwa mapema April 7 mwaka huu inaendelea kuwaunganisha pamoja wana habari ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
Ripoti ya Commonwealth Press of Journalists inasema jumla ya  wanahabari 58 waliouawa mwaka 2005 duniani,14 walihusika kwa kuandika habari zinazokemea rushwa.
Uhuru wa vyombo vya habari-mada zilizoandaliwa na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Manyara,
  • Nafasi ya waandishi wa habari katika kuleta maendeleo ya mkoa,
  • Usalama wa mwandishi wa habari ngazi ya mkoa,
  • Mdau wa mwandishi wa habari kushikikiana kuleta uhuru wa Habari.
Waandishi wa habari Tutaendelea kupigania uhuru wa vyombo vya habari na kusema ukweli mtupu."

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top