Mgodi
wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI
Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima
Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), na kuendesha harambee ya
kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.
Shughuli
hii inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya
Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la
ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya
wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima
Kilimanjaro .
Kilimanjaro
Challenge against HIV & AIDS ni mfuko unaochangia juhudi za
serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii
kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).
Kilimanjaro
Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya
nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya
Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii
inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.
Mfuko
huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba
na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro.
Takwimu
zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha
kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 %
mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko anasema, “
Mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na
VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku.
"Ugonjwa
huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji
kubadilisha hali hii. Lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia
serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri tatu.
"Sifuri
katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo
vitokanavyo na UKIMWI. TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa
Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge
tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha
mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
"Tuna
matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga
hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya
nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na
mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho
na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko.
“Watoto
watakaoshiriki katika zoezi la Kilimanjaro Challenge mwaka huu ni wa
kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 13. Watoto hao yatima kutokana
na tatizo la VVU/ UKIMWI wamesaidiwa na Kituo cha kulea watoto yatima
cha Moyo wa Huruma Orphanage Center kilichopo Geita.
"Changamoto
kubwa inayotokana na janga hili ni pamoja na maelfu ya watoto yatima
wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na
kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na
watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo."
Post a Comment
karibu kwa maoni