Watu
45 wamepoteza maisha katika kijiji kimoja jimbo la Kaduna nchini
Nigeria baada ya watu wenye silaha kuvamia kijiji hicho na kuchoma moto
nyumba.
Wahanga
wa tukio hilo wengi wao wanadaiwa kuwa ni wale wa kundi maalum
lililoundwa kwa lengo kulinda mifugo kijijini hapo kufuatia matukio
kadhaa ya wizi.
Imeelezwa
kuwa watu hao wenye silaha walizingira kijiji cha Gwaska majira ya
mchana na kuanza kurusha risasi hovyo huku wakichoma moto nyumba. Kila
aliyetaka kutoroka alishambuliwa vikali, kwa mujibu wa ripoti
iliyotolewa na BBC.
Serikali
ya Rais Muhammadu Buhari imeendelea kulaumiwa kwa kile kinachodaiwa
kutochukua hatua za kuridhisha kusitisha vitendo hivyo vya kihalifu
vinavyochukua maisha ya wananchi wasio na hatia.
Mwezi uliopita, wachimbaji wadogo wa madini 14 waliripotiwa kuuawa na watu wenye silaha katika eneo la Birnin Gwari.
Post a Comment
karibu kwa maoni