0
Rais Magufuli amewataka Wakulima na Wafugaji kuacha vitendo vya kupigana na kwamba katika serikali yake hakuna mtu aliyeko juu zaidi ya mwingine na kusisitiza kwamba watanzania wote ni sawa kwani ndiyo waliyomchagua.

Akizungumza jana na wananchi wa Morogoro akiwa njiani kuelekea Msamvu Raid Magufuli alisema kwamba kamwe vitendo vya kupigana visirudie katika serikali yake na kwamba wale watakaokiuka watashughulikiwa.

Aidha aliongeza kuwa anataka wakulima na wafugaji waishi kwa kuheshimiana kwani yeye anachokihitaji ni amani.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewashangaa Wafugaji kuwalisha ng'ombe mazao ya wakulima ilhali kuna majani ya kutosha na wanaposhtakiwa wanaamua kutumia gharama kubwa kuhonga hata kufikia hatua ya kuuza ng'ombe.

"Mimi nimekaa kwa wamasai Monduli, nimechunga mpaka ng'ombe za wamasai nikiwa JKT Makuyuni. Ni watu wazuri tu. Sasa kwanini wamasai wa huku wanachukia mali za wengine wakulima? Nataka niwaaeleze nitalifuatilia hili.

Pamoja na hayo aliongeza "Kama yupo mmoja ambaye analiisha kila siku anajifanya ana mali huyo mimi ndiye ntalala naye mbele mwenyewe".

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top