Serikali
imeagiza wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa biashara kufuatilia na
kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaopandisha bei ya sukari kwa
makusudi katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi wa mfungo wa Ramadhani.
Pia imetoa vibali kwa wafanyabiashara kuingiza sukari nchini ili kukubaliana na mfumuko wa bei ya sukari nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassimu
Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo
ambaye alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu mfumuko wa bei ya sukari
ambayo sasa umefikia Sh 3,200.
Akijibu
swali hilo, Majaliwa amesema tayari serikali imelitafutia ufumbuzi kwa
kulenga kuhakikisha upatikanaji wa sukari uwe wa kutosha na kila mwenye
mahitaji ya matumikzi aweze kupata bidhaa hii ikiwa wanaoanza mfungo,
“Ili
kuweza kufanya soko la sukari kuendelea kuwepo na kupunguza bei ya
sukari ya ndani, vibali tumeashaviagiza na tayari sukari imeanza
kuingia na bodi ya sukari kupitia wizara ya kilimo inaendelea kufuatilia
mwenendo wa uingiaji wa sukari nchini ili iweze kuifikia hadi ngazi ya
vijiji na huduma ipatikane maeneo yote.
“Niwaondolee
mashaka Watanzania hasa waislamu kwamba sukari itapatikana kipindi
chote cha Ramadhani na maeneo yote ambayo yanahitaji sukari kupitia
vibali tulivyotoa tutaendelea kufuatilia mwenendo wa bei ili watu
wasipandishe kwa makusudi, tutafanya ufuatiliaji kwenye maduka kwani
wakipandisha kwa makusudi watakuwa wanawaadhibu waislamu kwa sababu ya
kuwa na mahitaji makubwa,” amesema.
Post a Comment
karibu kwa maoni