Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC , Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matanshi wanayodai yameichafua klabu yao (Yanga) mbali na hili wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10
Kauli ya Ahmed iliyosababisha haya 👇
“Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae , Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza ..mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”
“Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia…kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code”
Demand letter ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao , hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini
Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)
1.Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake
2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 ( 10,000,000,000)
Yanga wamemaliza kwa kusema kama hayo maagizi hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi
Kutoka chanzo cha kuaminika.
Post a Comment
karibu kwa maoni