MTOTO Angela Lucas Abdul (13)[katika picha] anayesoma
shule ya msingi Matufa darasa la tano iliyopo kata ya Magugu wilaya ya Babati
mkoani Manyara anaesumbuliwa na tatizo
la Macho na ulegevu wa viungo vyake vyote hali inayomfanya ashindwe kuhudhuria
shule anaomba msaada kwa wasamalia wema.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha mtaa kwa mtaa cha Redio Manyara Fm Babati akiwa ameongozana na bibi yake Hadija Shabani katika ofisi za redio amesema kuwa mjukuu wake alizaliwa akiwa na afya nzuri baadae alianza kupatwa na matatizo hayo.
Bibi anasema kuwa mtoto angela
anao wadodo zake wawili ambao nao wanasumbuliwa na matatizo kama hayo.
Kutokana na hali hiyo mama wa
watoto hao ambao wote wanasoma inamlazimu kuwapeleka watoto shule asubuhi na
kuwapelekea chakula na kuwarudia tena baadae kuwachukua kwani hata kuvuka bara
bara au kukimbia hata kujificha wakati wa mvua ni vigumu kwao kutokana na
viongo vyao kulegea.
Bibi yake anasema msaada mkubwa anaoumba ni
msamaria mwema ajitokeze na kuwasaidia wajukuu zake wapate shule ya watoto wa
aina hiyo yenye bweni na kuwapatia matibabu na mungu atamlipa kwani yeye wala
mama na baba yao hawana uwezo.
Aidha bibi wa mtoto huyo anawaomba wasamaria wema kutoa mchango wao wa hali na mali ili afanikiwe kumpeleka Angela kwenye matibabu na kupata shule ya bweni,kiwango cha fedha kinachohitajika hadi sasa hajafahamu.
Kwa watakao guswa na tatizo la mtoto Angela
watoe michango yao kwa simu namba ya VODACOM M PESA 0756294847 ya bibi yake.
Post a Comment
karibu kwa maoni