0

Mgogoro wa kugombea maji umesababisha watu wasiojulikana kuweka kinyesi cha binadamu kwenye chanzo cha maji kinachotegemewa na wananchi zaidi ya elfu 50 wa vijiji saba vya tarafa ya Leguruki wilaya ya Arumeru mkoni Arusha kitendo kilichoibua taharuki na hofu kubwa na kusababisha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuhamia kwa muda katika eneo hilo kushughulikia tatizo hilo.
Baada ya kamati hiyo kuwasili katika eneo hilo viongozi wakamweleza mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo kilichosababisha na hatua walizochukuwa baada ya tukio hilo.
Mhandisi wa maji wa wilaya ya Arumeru Bi Happy Mrisho amesema mgogoro ni wa muda mrefu na ulishika kasi baada ya kuanza kwa mradi kusambaza maji hayo kwa wananchi wa vijiji vingine,madai ambayo yamepingwa vikali na wananchi hao.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Mrisho Gambo akatoa maelekezo na msimamo wa serikali ambayo yaliungwa mkono na wananchi wote na wakakubali kumaliza tofauti zao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top