BENNY MWAIPAJA-WFM,
DAR ES SALAAM
MAKAMU wa Rais wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB, Bw. Amadou Hott, ameahidi kuwa Benki yake
itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia ruzuku na mikopo yenye
masharti nafuu ili iweze kutekeleza malengo yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi
ya Viwanda katika kipindi kifupi kijacho.
Bw. Amadou Hott,
anayeshughulikia masuala ya Nishati na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi,
amesema Benki hiyo imetenga kiasi cha Dola Bilioni 12 kuzisaidia nchi za Afrika
ikiwemo Tanzania ili ziweze kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na vitendo
vinavyochangia mabadiliko ya Tabia Nchi.
Amemweleza Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alipokutana na kufanya mazungumzo naye
ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwamba kipaumbele kikuu ni kuhakikisha kuwa
sekta ya Nishati inaboreshwa hapa nchini kwa kuhuisha Shirika la Ugavi wa Umeme
nchini-TANESCO kuondokana na madeni makubwa yanayolikabili, ili liweze kuchochea uchumi na ukuaji wa
viwanda kwa kutoa huduma bora na kwa gharama nafuu.
Pause
Amesema kuwa Benki
yake pia imekuja na mkakati wa kuhimiza matumizi ya nishati jadidifu ili
kupunguza ama kuondoa kabisa matumizi ya kuni katika kupikia badala yake
matumizi hayo yaelekezwe katika kutumia nishati mbadala ili kuokoa kiasi
kikubwa cha miti na misitu inayoharibiwa nchini ambapo watafadhili miradi ya
matumizi ya nishati mbadala katika maeneo ya mijini na vijijini
Pause
Kwa upande wake,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, pamoja na mambo mengine, amepongeza
jitihada za Benki hiyo katika kuboresha miundombinu ya barabara hapa nchini na
amemwomba Makamu huyo wa Rais wa AfDB kusadia ujenzi wa Reli ya Kati kwa
kiwango cha Kimataifa, hatua ambayo itachangia kuimarisha sekta ya usafiri na
usafirishaji wa abiria na mizigo katika eneo lote la maziwa makuu
Pause
Mkutano kati ya
Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bw. Amadou Hott na
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, umehudhuriwa na maafisa
waandamizi wa Benki hiyo pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.
Post a Comment
karibu kwa maoni