0
Responsive image
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam , Simon Sirro
Jeshi la Polisi Kanda Maalum la DSM limezuia zoezi la usafi  lililopangwa kutekelezwa na Chama cha Wananchi CUF katika ofisi za chama hicho zilizopo BUGURUNI Jijini DSM.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam , Simon Sirro amewaambia Waandishi wa habari kuwa zoezi hilo limezuiliwa kwa sababu za kiusalama.
Aidha ,Kamanda Sirro amesema jeshi hilo linawashikilia Watuhumiwa saba kufuatia tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa  baadhi ya Waandishi wa habari na Wafusi wa CUF katika mkutano uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Wakati huohuo Kamanda Sirro ametangaza kukamatwa kwa magari matano ya wizi katika nyumba ya mkazi mmoja wa maeneo ya MBEZI jijini DSM, ambaye amekiri kujihusisha na wizi wa magari katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top