0
Responsive image
Mkoa wa Singida umetenga vituo mia moja tisini na saba kwa ajili ya kutolea chanjo kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanakamilisha chanjo zote muhimu ili kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Akizindua zoezi la  huduma ya chanjo kwa wajawazito na  watoto  chini ya miaka mitano Mkoani Singida, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Elias Tarimo amesema idadi kubwa ya wanaopatiwa chanjo hizo  huwa hawarudi tena kwenye vituo vya chanjo kumalizia chanjo zilizobaki.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida,Salum Manyatta ametoa taarifa ya kuwepo kwa tatizo hilo na amedai kuwa asilimia 12 ya watoto walipatiwa chanjo ya magonjwa matano ya Pepopunda, homa ya Ini, Dondakoo ,Mafua Makali na Kifaduro hawakurejea  kumaliza chanjo zilizobaki.
Mkoa wa Singida umetenga vituo mia moja tisini na saba  kwa ajili ya kutolea  za chanjo hizo kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top