Baada ya kusimama kwa muda wa wiki moja hatimae ligi daraja la 3 mkoa wa Manyara imeamishiwa katika mkoa jirani wa Arusha kutokana na hali ya kiusalama kutokuwa imara katika kituo ambacho kilikuwa kinachezwa michuano hiyo katika hatua ya nane bora ambayo ni mji wa Mirerani iliyoko Wilayani Simanjiro Mkoani hapo.
Taarifa hiliyotolewa Jana na jeshi la Polisi Mkoani hapo limetoa katazo la kuendesha Mashindano hayo ya ligi daraja la Tatu Ngazi ya mkoa kwa hatua ya nusu fainali 2016/2017 katika viwanja vyote vya Mirerani hadi hapo itakapo hakikishiwa usalama wa wananchi vinginevyo kamati ya Mashindano hayo imetakiwa kutafuta uwanja nje ya mji wa Mirerani ambapo itakuwa salama kwa wananchi.
Baada ya Taarifa hiyo kamati ya Mashindano ya ligi hiyo walikaa Jana Kwenye kikao na viongozi wa vilabu shiriki ambapo walikubaliana kutumia uwanja wa kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Akizungumza na mwandishi wa Blog hii Kennedy Luca, katibu wa kamati ya Mashindano ambae pia ndie msimamizi mkuu wa kituo cha Mirerani Nuru Mkireri hili kuzungumzia suala hilo ambapo amekiri jeshi la polisi kuleta barua ya katazo ya kutumia uwanja wa CCM -Mirerani kwa ajili ya mashindano hayo lakini pia akasema hata kabla ya hapo walikuwa na mpango wa kuiamishia ligi hiyo mkoani Arusha hili kuepusha lawama za Mashabiki wa timu zote na vurugu ambazo zilianza kujitokeza na kuwaomba mashabiki Soka Mkoa wa Manyara na Arusha kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid hili kushuudia michuano hiyo katika hatua ya nusu fainali.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Manyara Forunatus Kalewa akiongea na kipindi cha Manyara sports redio manyara fm amesema Ligi hiyo itaendelea leo katika hatua ya Nusu fainali katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ambapo itachezwa michezo miwili mchezo wa kwanza itakuwa kati ya Magugu Rangers ambao watacheza na Nyanza fc mchezo ambao utachezwa majira ya saa nane kamili za mchana na mchezo wa pili utachezwa majira ya saa kumi na Nusu za jioni ambapo itazikutanisha timu ya Mererani sports na Songa fc.
Ligi Ya soka Mkoani Manyara ilisimama kwa takribani wiki moja baada ya kutokea mgogoro mkubwa baada ya timu ya usalama ya Babati kuikatia rufaa timu ya Songa fc ya Mirerani Wilayani Simanjiro wakidai kuwa walimchezesha mchezaji Amir Peter ambae alikuwa bado anausajili na timu ya Madini fc ya jijini Arusha hivyo kamati ya Mashindano ilikaa na kuamua kuiengua timu ya Songa lakini kosa kubwa lililofanywa na kamati hiyo ni kutoa maamuz upande mmoja bila kuwashirikisha upande wa walalamikiwa na bila kuwapa barua ya Kuwaengua katika mashindano hali ambayo ilipelekea timu Tatu kufika katika Pre match meeting na kuzua tafrani kubwa na kufanya Kamati ya Mashindano kuamua kusimamisha ligi hiyo.
Lakini kamati Ya rufaa ya mkoa ilikaa tena na kupitia rufaa walioikata timu ya U salama dhidi ya Songa ambapo waligundua kuwa haikuwa na mashiko hvyo waliamua kuirudisha Songa fc na kuamua kuwaondoa tena Usalama fc ya Babati.
Post a Comment
karibu kwa maoni