0
Kwa kitendo alichikifanya cha kumtolea maneno ya matusi spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai sasa kamati ya maadili inamuhitaji kumhoji Mheshimiwa Halima Mdee Mbunge wa Kawe..
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
Spika wa Bunge la Jamuhuri Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Kawe Halima Mdee kuripoti katika Kamati ya Maadili Kinga na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu wakati uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ukiendelea.

Spika Ndugai amesema  leo majira ya saa tano Mbunge huyo anatakiwa awe tayari ameripoti katika kamati hiyo.

Ndugai ametoa agizo hilo bungeni Mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top