0
Usindikaji wa Matunda.
Vijana 32 waliopatiwa mafunzo ya usindikaji vyakula na vinywaji wilayani Hanang’ mkoani Manyara wamesema ujuzi huo utawawezesha kuanzisha miradi midogo ya usindikaji na kujikwamua kiuchumi.

Mafunzo hayo yameendeshwa na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Manyara kupitia mradi wa fursa kwa vijana kwa lengo la kuwapatia ujuzi wa ujasiriamali vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 30.

Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Manyara Joseph Mwingira ameomba Halmashauri kuwakopesha vijana hao fedha za mitaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Manyara kupitia mradi wa fursa kwa vijana linatarajia kuwafikia zaidi ya vijana 250 katika awamu ya pili ya kuwawezesha vijana kiuchumi katika wilaya ya Hanang.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top