Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Rais Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani Kilimanjaro kuanza ziara ya siku Tatu ambapo pamoja na mambo mengine atakua mgeni rasmi katika Sherehe za Wafanyakazi Mei Mosi.
Akizungumzia ziara hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick ametoa wito kwa Wakazi wa mkoa huo kujitokeza kumlaki Rais Magufuli pamoja na kushiriki katika sherehe hizo.
Akiwa mkoani Kilimanjaro, Rais Magufuli pia atafanya kikao na viongozi wa dini wa mkoa huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni