0
Mkazi wa Kijiji cha Magara Babati Manyara  akivuka mto.picha na John Walter
SERIKALI imeahidi kutopoke amradi wa bara bara ya Manyara- Dodoma  inayojengwa kwa kiwango cha lami endapo mkandarasi atashindwa kutimiza ujenzi kwa kiwango kama walivyokubaliana kwenye mkataba wao.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Manyara Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa lengo la kutembelea ujenzi huo  mara kwa mara ni kuhakikisha Mkandarasi anafanya kazi yake kwa kiwango kinachokubalika.
Kulia ni Meneja wa wakala wa Bara bara mkoa wa Manyara [TANROADS] Mhandisi Bashiru R.Rwesingisa akiwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa. Picha na John Walter

Profesa Mbarawa ameeleza kwamba barabara hiyo inayoanzia Bonga –Mela yenye urefuwa kilomita 88.8 iliyogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 83.3 mpaka sasa imeshakamilika kwaasilimia 76 na kwamba kimebaki kipande chenye urefu wakilomita 18 kwaupandewaManyara.

Aidha amefafanua kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha barabara hiyo inakamilika baada ya miezi sita (6) na ifikapo mwezi Octoba mwaka huu kuzinduliwa rasmi na kuongeza kuwa ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanaweka ulinzi wa kutosha baadaya barabara hiyo kukamilika.

Pia ametoa shukrani kwa Tanroads kwa mikoa hiyo pamoja na Mkandarasi kwa ujenzi ambao unaonyesha utakamilika kwa wakati unaotakiwa na ambao upokatika viwango vinavyokubaliwa, hivyo wananchini bora wakailinda kwanini kilio chao cha muda mrefu.

“Barabarahiiitakuwaukombozimkubwa kwawana nchi kwani itawapunguzia muda wa kusafiri napiaitawapa fursa zakibiashara kati ya Mikoa hii miwili, hivyo nilazima wailinde ili isiharibiwe na watu wanaong’oa alama za barabarani na kuharibu barabara kwama kusudi, hatua kali zakisheria zitachukuliwa kwa atakaebainika” alisisitizaMbarawa.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wadaraja la Magara linalounganisha wilaya za Mbulu na Babati alisema Zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa daraja hilo inatarajiwa kufunguliwa tarehe 28 mwezi Aprili ambapo tayari serikali imekwishatenga malipo ya awali kwa ajili ya malipo ya mkandarasi atakaepatikana.

Katika bajeti 2017/2018 serikali itahakikisha inatenga fedha zakukamilish aujenziwadaraja hiloambalo ni muhimu nategemezi kwa wakazi wawilaya zotembili na watalii wanaoingia katika hifadhi ya ziwa Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta Joel Bendera alisema kuwa mkoa utaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha mkandarasi anakamilisha kazi hiyo kwa wakati na viwango vitakavyokubaliwa katika mkataba wa kazi hiyo.

Baadhi ya Wakazi na wa Magara na Mayoka pamoja na wanapita katika mto huo Wanannchi wakizungumza na Blog hii walisema  adha wanayokutana nayo katika mto huo ni kubwa  haswa katika kipindi hiki cha mvua na kuitaka  serikali ifanye haraka kuwajengea daraja hilo na sio kuwapa ahadi ambazo si za kweli kwani limekuwa ni kero kwa muda mrefu.

Nao Wanafunzi wakizungumza na John Walter  wamesema kukosekana kwa daraja muda mwingine wanashindwa kuhudhuriashule hivyo  kupelekea kufanya vibaya katika masomo yao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top