Elimu ni
ufunguo wa Maisha,Elimu ni urithi wa leo na sio mali kama ilivyokuwa hapo
zamani.
Kila mwanafunzi
anayekuwepo masomoni lengo lake kubwa ni kufanya vizuri ili aweze kufika katika
malengo Fulani aliyojiwekea.
Ndoto hizo
zimekuwa kinyume kwa Mwanafunzi Selina Songay Isaay aliyekatisha masomo yake
akiwa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Komoto iliyopo Halmashauri ya
mji wa Babati mkoani Manyara kwa ugonjwa ambao umekuwa ni kitendawili kwake
kwani haijulikani ni nini haswa kinachomsumbua binti huyo.
Selina
akizungumza na Johnwalter Blog amesema kuwa alifika hospitali na kuambiwa kuwa
analo tatizo la Goita ila anachokishangaa ni kushindwa kutembea umbali mrefu na
kuona vitu vya ajabu ajabu.
Anasema kuna
muda akifika bafuni kuoga anaomuona nyoka mkubwa nyuma yake hali inayompa
wasiwasi na hofu kubwa katika maisha yake.
Nimezungumza
na Selina muda mrefu huku akibubujikwa na machozi hali kwani ndoto zake kubwa
ni kusoma.
SELINA
anaomba msaada ili akafanyiwe upasuaji
katika hospitali ya rufaa ya Kcmc Moshi kwa mujibu wa maelezo aliyopewa na
daktari na aendelee na masomo yake ndoto zake zitimie.
MSIKILIZE KWA KUBOVYA HAPA.
Post a Comment
karibu kwa maoni