0
Image may contain: 2 peopleSerikali ya Burundi imewapa muda hadi mwisho wa mwaka watu walioko kwenye mahusiano ya kimapenzi ambao hawajaoana kuhalalisha ndoa zao.
 Agizo hilo linafuatia kampeni ya Rais Pierre Nkurunziza ya kile kilichotajwa kuimarisha maadili ya jamii.
 Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema Burundi inakumbwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu kutokana na ndoa zisizo halali, ndoa za mitala, watu kuwa na wake wawili na mamia ya wasichana wa shule kubeba uja uzito.
Serikali ya Burundi imesema ndoa za kanisani na za kiserikali ndiyo suluhisho na wajibu wa kitaifa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top