Baada ya Kikosi cha klabu ya Yanga kutua kwa kishindo ndani ya Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania may 25 na kuibua shangwe na nderemo kutoka kwa
wabunge mashabiki wa timu hiyo wakati wakitambulisha kombe walilotwaa la ligi kuu vodacom Tanzania Bara {VPL}.
Leo mabingwa hao mara ya 27 wametua mjini Babati mkoani hapa wakitokea Dodoma ambapo mashabiki walijitokeza kwa wingi kuwashuhudia na kupata nafasi ya kupiga picha za kumbukumbu na mastaa wa yanga.
Wachezaji wa Yanga
walioongozana na uongozi mzima wa timu akiwemo Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa Master na wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki jijini Arusha keshokutwa dhidi ya Arusha Football Association [AFC] na baadaye wataelekea Simanjiro katika mji mdogo wa Simanjiro kucheza michezo Mingine ya kirafiki na kutembelea migodi ya Tanzanite one.
Huko mererani wamealikwa na mwenyekiti wa AFC Charles Mnyalu.
Baada ya utambulisho wa msafara wa wachezaji wa Yanga waliondoka na kuelekea jijini Arusha.Nahodha
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alizungumza na redio Manyara Fm na kueleza
furaha waliyonayo baada ya kupata ushindi kwa mara nyingine huku yeye
akiwa nahonda wa timu hiyo.MSIKILIZE HAPA CHINI
Pia mashabiki walipiga picha na kombe wakijivunia ushindi.
Post a Comment
karibu kwa maoni