Hafla
ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala,
Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo
Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi
wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.
Mradi
wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia
kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya
watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.
Hivi
Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya
mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba
Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo
yatapitishwa katika bomba hilo hilo.Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Bw. George Masaju (kulia) na Mwanasheria wa Uganda Bw. Milliam Byaruhanga (kushoto), wakionesha nakala za Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda. |
Post a Comment
karibu kwa maoni