0
Tunaitaka Serikali kupitia Bunge, kutunga Sheria kuzuia Ukatili wa Kijinsia.Jiunge Nasi!

Ndugu Mtanzania,
 
Ukatili wa kijinsia ni janga la kitaifa na lina athari kubwa Katika Maendeleo ya taifa na hatua madhubuti zisipochukuliwa basi tunu kubwa za taifa letu ikiwemo utu na heshima zitakuwa matatani. Ukatili wa kingono, vipigo, mila kandamizi, ukatili wa majumbani, ukatili wa kiuchumi, udhalilishaji wa kimwili vyote hivi ni baadhi tu ya aina za ukatili ambao umeendelea kukiuka misingi ya haki za binadamu na haki za wanawake hapa nchini.
• Je wajua Ndoa za Utotoni ni 37% hapa nchini? Na kwamba kati ya watoto wa kike 5 wawili huozeshwa kabla ya kutimiza miaka 18?
• Je wajua wasichana wanaopata mimba mashuleni ni 26%?• Je wajua vikongwe takribani 124 waliuwawa kati ya Julai 2015 and Machi 2016 na kufikisha idadi ya vikongwe 1,423 waliouwawa kuanzia 2013 hadi 2016?
• Je wajua katika jiji la Dar es Salaam kwa wastani wanawake au wasichana 3 walibakwa kila siku kwa mwaka 2016?
• Je wajua kesi 5,802 za ubakaji ziliripotiwa mwaka 2015 na hii ni sawa na wastani wa wanawake 483 walibakwa kila mwezi, ikimaanisha kuwa angalau wanawake au wasichana 16 walikuwa wanabakwa kila siku hapa nchini?
• Je wajua kwa wastani matukio 1400 ya Ukatili kwa wanawake yalitokea kila mwezi kwa mwaka 2015?Aibu Aibu Aibu! 
Matukio haya na mengine mengi ni aibu kwa taifa na ni ukiukwaji wa haki za binadamu na haki za makundi.
Hivyo basi kwa kutambua misingi hii tunakuomba ndugu Mtanzania uungane nasi kuitaka serikali kwa kupitia Bunge letu kutunga sheria ya kupinga ukatili wa kijinsia ambayo itawezesha kudhibiti janga hili.
Uwepo wa sheria hii itasaidia kudumisha Amani majumbani na hata kwenye taifa kiujumla na hivyo kuwezesha wanajamii kushiriki kikamilifu katika shughuli za Maendeleo na uzalishaji Kiuchumi.
Ndugu Mtanzania kila mmoja wetu ana nafasi kubwa Katika kulinda misingi ya haki na usawa na kuweka ulinzi kwa wanajamii wote wanawake na wanaume.Tafadhali tumia dakika moja tu kuweka sahihi yako ya kutaka kuwepo kwa sheria hii ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Pamoja tuondoe ukatili wa kijinsia.
Weka sahihi yako Sasa!

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top