0
 
Zikiwa zimebaki siku mbili kufika mwezi July kusitishwa kwa biashara ya mkaa,wafanyabiashara wa biashara hiyo wilayani Babati wameiomba serikali ilegeze sharti hilo.
 Wafanyabiashara kwa nyakati tofauti wakizungumza na kituo cha redio MANYARA FM wamesema kuwa watakaoathirika na hatua hiyo ni wafanyabiashara wa chakula kama Mama Ntilie na wenye Hotel kwa kuwa bidhaa hiyo itakuwa inapatikana kwa shida.
Hivi karibuni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alitangaza mabadiliko katika biashara ya mkaa nchini na kusema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu hakuna mkaa wowote utakaosafirishwa kutoka wilaya moja kwenda nyingine Wafanyabiashara wa mkaa wamelaumu kauli hiyo.ili kunusuru misitu inayoteketea kwa kasi hapa nchini.

Aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 24 wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma.

“Kuanzia mwezi Julai hakuna ruhusa ya kutoa vibali vya kuhamisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, mkaa utachomwa, utauzwa ndani ya wilaya kwa ajili ya matumizi ya Watanzania wanaohitaji nishati ya mkaa, lakini biashara ya mkaa ya kutoa Dodoma kwenda Dar es Salaam mpaka Zanzibar marufuku.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top