
Mkurugenzi
wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali
kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza
Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua
za kisheria watu wenye tabia hiyo.
Hayo
yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii
kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki
nchini.
Boaz
amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka kwa udi na uvumba
mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.
Na
amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha
kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha
madhara makubwa katika jamii.
”Kabla
ya kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika wa vyanzo vyako, wahsuika
wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa ya msingi”. amesema Boaz.
Aidha
waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy
Mwalimu ametaarifiwa na Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna
mchele wa aina hiyo nchini.
Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.


Post a Comment
karibu kwa maoni