
Baada
ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuwasili katika ofisi ya
mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, kama alivyotakiwa kufanya
Juni 29, ameruhusiwa kuondoka na kutakiwa kurudi tena Alhamisi ijayo.
Mwanasheria
wa Lowassa, Peter Kibatala amezungumza na waandishi wa habari na kusema
kuwa Lowassa ametakiwa kurudi Alhamisi bila sababu za kuahirishwa kwa
mahojiano hayo kuwekwa wazi.
“Hatujaambiwa kwa nini ila tumeambiwa tuje alhamisi ijayo kwa ajili ya maelekezo na kuwasikiliza zaidi,” alisema
Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kwenda katika ofisi za DCI ambako anahojiwa kwa tuhuma za uchochezi.
Lowassa
ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alihojiwa Juni 28 na Juni 29
na Wakili Kibatala alizungumza na wanahabari mara baada ya mahojiano
hayo.
Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya kichochezi Juni 23, mwaka huu katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Post a Comment
karibu kwa maoni