![]() |
Wadau wa Maendeleo mkoa wa Manyara wakisikiliza mada mabalimbali zinazowasilishwa. |
![]() |
Wadau wa
Maendeleo mkoa wa Manyara wakisikiliza mada mabalimbali zinazowasilishwa.
|
July 10 2017, wadau
wa Maendeleo wa Halmashauri ya mji wa Babati walikutana na kuajadilim
amafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango na bajeti kwa mwaka 2016/2017
kwa ajili ya Maendeleo y mji wa Babati.
Katika
hotuba ya Katibu tawala wa Mkoa wa Manyara Eliakim Maswi iliyosomwa na katibu
tawala wilaya ya Babati imeeleza kuwa Halmashauri ilipanga na kutumia
Tshs.3,193,04,083/= za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ikijumuisha
mapato halisi Tshs 2,964,012,797 ysiyo na masharti na Tshs 229,027,286/= mapato
yenye masharti.
Taarifa hiyo
ilieleza kuwa hadi kufikia mwezi Juni,2017 Halmashauri ilikusanya jumala ya
Tshs 1,476,980,365= ya mapato halisi sawa na asilimia 46 ya makisio ya mapato
yote ya ndani ikijumuisha Tshs
288,008,578/= za mapato yenye masharti na Tshs 1,188,971,786/= ya mapato
yasiyo na masharti.
Nimefahamishwa
kuwa kutakuwa na mada itakayowasilishwa
ambayo itaonesha kwa kina maeneo ambayo tumefanya vizuri licha ya
changamoto za kibajeti zilizojitokeza.Bajeti hii tuliandaa kwa pamoja hivyo ni
vema tukajadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza kwa pamoja ili kujua ni
jinsi gani tunajipanga kwa mwaka 2017/2018
Ndugu wadau,
ni ukweli usiopingika kuwa serikal pekee haiwezi kufanya kila kitu,ndio maana
inasisitiza ushiriki wa wadau/sekta binafsi katika shughuli za maendeleo ,
hivyo mahusiano kati serikali kuu,serikali za mitaa na sekta binafi/wadau
lazima yaboreshwe
Napenda
kuwafahamisha kuwa maendeleo yoyote duniani hayawezi kuletwa bila kuwepo na
amani,nawasihi wote mlioko hapa kwa niaba ya wasiokuwepo humu ukumbuni kuwa
mabalozi wazuri wa kuilinda na kuitetea amani yetu kwa nguvu zetu zote Nawaomba
mzingatie kwa makini mada zitakazoletwa ili muweze kutoa michango yenu
itakayoitoa Halmashauri yetu hapa tulipo nz kuifikisha katika hali bora zaidi
Ni vizuri
halmashauri yetu ikachangia kikamilifu katika azma ya serikali ya awamu ya tano
ya kuifikisha nhi yetu kuwa nchi yenye
uchumiwa kati ifikapo 2020.
kwa pamoja
tulijenge babati yetu.
nawashukuru
sana kwa kunisikiliza na kikao chetu nimekifunga rasmi.
ELIACKIMU C. MASWI
KATIBU TAWALA MKOA
WA MANYARA.
Post a Comment
karibu kwa maoni